Ni ukweli usiopingika kwamba suala la kupendeza na kuonekana nadhifu mbele za watu ni zuri na hukubalika katika jamii yetu na duniani kote,LAKINI akina dada mnapaswa kuwa makini sana mnapokuwa katika harakat za kuweka au kuvaa miilini mwenu mapambo yoyote yale yauzwayo sokoni kwa maana wengi wenu hawatambui mahali yalipozalishwa wala malighafi zake hawazijui.
Basi leo nitazungumzia mapambo haya yatumiwayo sana na akina dada wengi ambayo inawezekana yakawa ni hatari sana kwao katika ulimwengu wa kiroho,mapambo hayaa ni wigi na nywele zijulikanazo kama rasta.
Kuna hekalu lililoko kusini mwa india lijulikanalo kama hekalu la telopati,hekalu hili ni mojawapo ya mahekalu inayovutia idadi kubwa ya watu zaidi duniani hata kushinda miji ya jerusalem na mecca.Kila mwaka kati ya watu milioni arobaini na hamsini huzulu hekalu hii kumuabudu mungu wa kihindu anayefahamika kama venkateshwala,nusu ya mahujaji hao hukata nywele zao na kumpa mungu huyu.
Kutokana na hili hekalu hii ya telopate ni kituo kinachokusanya kiasi kikubwa zaidi cha nywele za watu duniani,wasimamizi wa hekalu hii hukusanya tani 500 za nywele kila mwaka, kila mwezi nywele hizi huuzwa katika minada na mitandao,takwimu zinaonesha kuwa hekalu hii hukusanya dola milioni 4 kila mwaka kutokana na uuzaji wa nywele hizi.
Mahujaji huketi kwenye foleni huku vinyozi wao wakiwa nyuma yao katika eneo maalum linalojulikana kama kalya nhkata(yaan mahala pa furaha).Katika hali ya kawaida nywele ni sehemu ya maisha kwa akina mama na akina dada nchini india.Wao hutumia muda mwingi kutunza nywele zao tena ni jambo la ufahari kwa mwanamke yeyote nchini india kuwa na nywele ndefu kwa sababu ni ishara ya urembo na uamuzi wao wa kukata nywele ni ishara ya unyenyekevu na kujitolea kwa mungu huyo(yan hutoa nywele zao za kwa mungu huyu kama sadaka).Baada ya kukatwa nywele zao na mahujaji,wanawake hao hutarajia mema kutoka kwa mungu huyo.
Nyingi kati ya nywele bandia zinazouzwa barani Afrika huagizwa kutoka India,India ndilo taifa linalouza kiasi kikubwa zaidi cha nywele za binadamu duniani,nywele hizi zinazouzwa kutoka hekalu huitwa remi na inakisiwa kuwa bora zaidi duniani na wanasema kuwa nywele na bei ya juu zaidi ni ile iliyojikunja kiasili kutoka kwa kichwa cha mama na kila moja ya nywele huuzwa kwa dola 1200 hivi.
Kwahiyo sasa,baada ya nywele hizo kukatwa hekaluni husafirishwa hadi kiwanda cha kimataifa rahel mjini chenai,afisa mkuu wa kiwanda hiki anaelezea kuwa nywele hizi za binadamu hugeuzwa na kupambwa ili kuuzwa kama nywele za kofia(wigi),nywele hizi huwekwa pamoja kisha zinachukuliwa na kukaguliwa vyema na kwao huonekana kama dhahabu,kila sehemu ya nywele huonekana na thamani kubwa na hii ndio dhahabu yao.
Baada ya nywele hizi kupangwa huoshwa mara 12 na maji ili kuhakikisha zinasalia safi kama zilivyokuwa kwenye vichwa vya akina mama kisha zinaachwa kukauka na kufungwa tayari kwa kupelelekwa sokoni hasa za nchi za Afrika.
Hatua ya akina dada kutumia nywele wasizojua zitokako kama mapambo mfano hizi zitolewazo kama sadaka kwa mungu wa kihindu kisha kutengenezwa na kusafirishwa kwetu afrika zina athari kubwa sana katika maisha yao ya kiroho na kimwili pia na ndio maana tafiti nyingi zilizofanywa zinaonesha asilimia kubwa ya wanawake wengi hutekwa na mapepo,majini na roho zingine chafu ambapo kisababishi mojawapo ni kutumia/kuvaa baadhi ya mapambo ambayo hapo awali yalitolewa kwa miungu wapinga KRISTO.Kwahiyo mimi binafsi nawasihi akina dada mtafakar sana kuhusu mapambo hayo mtumiayo na mchukue maamuzi yatakayokuwa na tija katika maisha yenu na familia zenu. ASANTENI SANA!
NB;
Chanzo cha habari hii; BBC
Taarifa hii ni ya ukweli kabisa wala sio hadithi kama wengine wanavyodhani
Ingia link hii uone jinsi wanavyofanya:
Hair Sacrificed to Idols!? https://youtu.be/AuduHfSRFiA via YouTube
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni