Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo JAMII. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo JAMII. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 11 Novemba 2016

BIRTH CERTIFICATE


Fahamu taratibu za kupata cheti cha kuzaliwa:
Kwa mujibu wa sheria unaweza kupata cheti katika Wilaya uliyozaliwa au katika ofisi za Msajili Mkuu, Makao Makuu ya RITA katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Tafadhali fika katika ofisi zetu, utatakiwa kujaza fomu BD 15 halafu utaambatisha kiambatishi kimoja kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha kupigia kura (2005), pasi ya kusafiria, cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondary (leaving certificate), cheti cha ubatizo. Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa hapo utakiambatanisha kwenye fomu yako utakayoijaza halafu msajili atapitia maombi yako yakiwa sawa utaandikishwa.
 

Jumatatu, 7 Novemba 2016

RITA

Picha ya RITA Tanzania

Je wewe ni mwanandoa??
umeshajisajili na kupata cheti cha ndoa kutoka RITA?
Mahitaji / taratibu:
Wasilisha nakala ya cheti cha Ndoa au maelezo juu ya Ndoa (majina ya wanandoa, tarehe ya ndoa na mahali palipofungiwa Ndoa)..
Wasilisha namba ya kuingizwa kwenye daftari la Ndoa....
Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 20000/=).


Alhamisi, 3 Novemba 2016

HOW TO GET BIRTH CERTIFICATE

Fahamu utaratibu wa kupata cheti cha kuzaliwa kwa watoto wenye umri nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10:
Jaza na wasilisha fomu BD15 (ijazwe na mzazi au mlezi)
Bandika picha ya mtoto(passport size)ambaye kizazi chake kimeombewa kusajiliwa.
Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono maelezo yako kwenye fomu.nyaraka hizi ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama... ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
Lipia ada inayotozwa (ada ya sasa ni shilingi 4000/=)