Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UCHUMI NA BIASHARA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UCHUMI NA BIASHARA. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 19 Desemba 2016

TANZANIA NA OIC: Lijue lengo kuu la Azimio la Abuja


                                         
WATANZANIA wengi kama mimi tulikuwa tukisikia tu kuhusu Azimio au Tamko la Abuja na Sheria za Kiislamu. Azimio hilo lilifanyika nchini Nigeria katika mji wa Abuja, mwaka 1989 ndiyo maana linaitwa Azimio la Abuja. Jumatatu ya Machi 12, mwaka huu, katika pita pita mjini Nairobi nimebahatika kupata gazeti linaloitwa " The ministry".
Katika gazeti hilo nikaona kwa mbali neno "Abuja declaration  and the Sharia law."  Nikalinunua gazeti hilo. Baada ya kulisoma, nikaridhika na nikaunganisha na yanayotokea katika nchi yetu ya Tanzania, juu ya harakati za wenzetu Waislamu ikiwa ni utekelezaji wa tamko hilo muhimu la Abuja.
Tamko au Azimio la Abuja linahusu nini hasa? Kadiri ya maelezo katika internet na gazeti hilo, inaonekana wazi kuwa Azimio la Abuja ni tamko rasmi juu ya Uislamu barani Afrika (Islam in Africa). Kwa hivi tunaweza kusema au tunasema kwamba  hili tamko lilitolewa katika kilele cha kongamano la Uislamu barani Afrika. Kongamano hili liliandaliwa na nchi 46 za Kiislamu zinazojulikana kama OIC (Organization of Islamic Conference).
Lengo la umoja huu ni kuuendeleza Uislamu barani Afrika, kutekeleza mikakati ya kiislamu na kutatua matatizo yanayolikabili Bara la Afrika kama vile ukimwi, kifua kikuu, njaa na majanga mengine. Lakini pia inasemekana hata kuona maadili yanafuatwa katika bara hili. Haya si mambo mabaya lakini swali la msingi ni; je, kwa kutumia sheria gani?
Inadaiwa kwamba katika yote hayo lengo kuu la OIC na hasa kupitia Azimio la Abuja ni kuona kwamba Bara lote la Afrika linakuwa la kiislamu. Huu ndiyo ukweli wa mambo na wala si uchochezi wala propaganda, ukitaka ukweli nenda tu kwenye internet utaupata najisomee maandishi mbalimbali juu ya umoja huo wa nchi za kiislamu, yaani OIC.
Kama mwandishi wa habari (mwanataaluma kamili) kazi yangu ni kuelimisha umma na si kuupotosha kamwe. Inaonekana wazi kwamba umoja  huu wa nchi 46 za kiislamu, sijui kama Tanzania imejiunga au bado lakini OIC ndiyo mwakilishi  na mzungumzaji wa masuala ya pamoja yanayohusu Waislamu barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.
Sehemu ya madhumuni ya OIC, kupitia Azimio au Tamko la Abuja ni; "kufuta katika hali zote imani ya dini isiyo ya kiislamu katika nchi wanachama. Na imani ambazo itabidi zifutwe ni dini ya kikristo, na nyinginezo ambazo hazikubaliani na imani ya kiislamu.
Kwa mantiki hii, ni dhahiri kwamba kama Tanzania itajiunga na Umoja huu wa  nchi za kiislamu itabidi dini nyingine zisizokubalika kwa imani ya kiislamu basi zifutwe. Sasa swali; je, hapa kuna uhuru wa kuabudu kweli? Na kama nia ya kutaka Tanzania ijiunge huko ni dhahiri Katiba yetu ya Tanzania ni lazima ibadilishwe kwanza, kwa sababu kwa sasa hairuhusu.
Lakini kwa upande mwingine, madhara ya Azimio hili la Abuja tunayasikia mara nyingi nchini Nigeria ambako Wakristo wengi wamekwishauawa kikatili; je, hii ni halali?
Ukichunguza kwa kina unaweza kubaini kwamba utekelezaji wa Azimio la Abuja unakuja pole pole, hauna haraka. Na ninasema wazi kwamba katika uchunguzi wangu nchini Tanzania, mipango hii pia imeanza kutekelezwa kimya kimya na kwa uangalifu mkubwa sana.
Hata hivyo, kwa namna ya kipekee mambo yameshajulikana juu ya ajenda hii ya siri, Mungu hawezi kuruhusu jambo la namna hiyo kutokea katika ardhi ya Watanzania.
Alama za Azimio hilo la Abuja zimeshaanza kujitokeza kwa mbali katika nyanja mbalimbali nchini Tanzania na kwa hiyo, wale wanaoshabikia suala la Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) kwanza wajue malengo yake ni  yapi. Na  ni vema kujiuliza je, Katiba ya nchi yetu, historia ya nchi yetu, utamaduni wa nchi utaweza kuukaribisha umoja kama huo?
Misingi iliyowekwa na muasisi na Baba wa Taifa Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Julius K Nyerere ilikuwa ya busara, upendo, usawa, inayokuza haki na amani kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote. Sasa fikiria kama ni kweli lengo kuu ndilo hilo je, Azimio la Abuja lina maslahi gani kwa Watanzania wa leo hii? Kama nilivyosema sifanyi propaganda bali ni kutaka kuelimisha umma wa Watanzania kama mwandishi hii ndiyo kazi yangu, kuwapa watu mwanga wajue wanakwenda wapi.
 Pia kama padre ni nabii wa kutahadharisha waumini na wananchi kwa ujumla juu ya mambo mbalimbali na kinyume cha hapo, wito  wangu hautakuwa na maana kabisa.
Yesu aliwaambia mitume wake; "Ninyi ni chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu" (Mathayo 5: 13-16). Nisipotimiza wajibu huu kutoka kwa Bwana basi mimi nitakuwa sijitendei haki mbele ya mwenyezi Mungu na mbele ya Watanzania wenzangu ambao wengi hawajui nini kinaendelea kuhusiana na masuala ya jamii na siasa.
Namaliza kwa kusema kwamba, sisi Watanzania na Tanzania yetu ni vema tukaendelea kushikilia misingi iliyojengwa na Baba wa Taifa kama tunataka kuendelea kuishi kwa umoja, upendo, haki na amani.
Nitaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusiana na Azimio la Ubuja katika makala zijazo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki mawazo ya Mwalimu Nyerere, Mungu wabariki viongozi wa Tanzania. Nawatakieni uchaguzi Mwema huko Arumeru Mashariki, chagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

AJIRA NA KAZI: KINACHOWASHINDA WENGI KWENYE USAILI WA AJIRA






Kuna kauli ya busara isemayo; kama hujajiandaa kushinda, ni wazi umejiandaa kushindwa.
Wengi tunaposhindwa, tumekuwa wepesi wa kutafuta sababu na visingizio, badala ya kutenga muda na kutafakari sababu ya kushindwa ili tutafute ufumbuzi.
Mtazamo huu unawagusa watu wengi wanaotafuta ajira na kujikuta wakitoka kapa.
Kuna sababu nyingi zinazowafanya watahiniwa wengi kushindwa kwenye usaili
Makala haya yatajadili sababu hizo na kupendekeza njia mwafaka za kukabili tatizo hili linalowakumba wahitimu wengi nchini.http://www.mwananchi.co.tz/…/1597592-3416774-6gk…/index.html

Ijumaa, 14 Oktoba 2016

JE,AKINA DADA NA AKINA MAMA MNAJUA RASTA NA WIGS MNAZOTUMIA KAMA MAPAMBO ZINAKOTOKA?



Ni ukweli usiopingika kwamba suala la kupendeza na kuonekana nadhifu mbele za watu ni zuri na hukubalika katika jamii yetu na duniani kote,LAKINI akina dada mnapaswa kuwa makini sana mnapokuwa katika harakat za kuweka au kuvaa miilini mwenu mapambo yoyote yale yauzwayo sokoni kwa maana wengi wenu hawatambui mahali yalipozalishwa wala malighafi zake hawazijui.
Basi leo nitazungumzia mapambo haya yatumiwayo sana na akina dada wengi ambayo inawezekana yakawa ni hatari sana kwao katika ulimwengu wa kiroho,mapambo hayaa ni wigi na nywele zijulikanazo kama rasta.
Kuna hekalu lililoko kusini mwa india lijulikanalo kama hekalu la telopati,hekalu hili ni mojawapo ya mahekalu inayovutia idadi kubwa ya watu zaidi duniani hata kushinda miji ya jerusalem na mecca.Kila mwaka kati ya watu milioni arobaini na hamsini huzulu hekalu hii kumuabudu mungu wa kihindu anayefahamika kama venkateshwala,nusu ya mahujaji hao hukata nywele zao na kumpa mungu huyu.
Kutokana na hili hekalu hii ya telopate ni kituo kinachokusanya kiasi kikubwa zaidi cha nywele za watu duniani,wasimamizi wa hekalu hii hukusanya tani 500 za nywele kila mwaka, kila mwezi nywele hizi huuzwa katika minada na mitandao,takwimu zinaonesha kuwa hekalu hii hukusanya dola milioni 4 kila mwaka kutokana na uuzaji wa nywele hizi.
Mahujaji huketi kwenye foleni huku vinyozi wao wakiwa nyuma yao katika eneo maalum linalojulikana kama kalya nhkata(yaan mahala pa furaha).Katika hali ya kawaida nywele ni sehemu ya maisha kwa akina mama na akina dada nchini india.Wao hutumia muda mwingi kutunza nywele zao tena ni jambo la ufahari kwa mwanamke yeyote nchini india kuwa na nywele ndefu kwa sababu ni ishara ya urembo na uamuzi wao wa kukata nywele ni ishara ya unyenyekevu na kujitolea kwa mungu huyo(yan hutoa nywele zao za kwa mungu huyu kama sadaka).Baada ya kukatwa nywele zao na mahujaji,wanawake hao hutarajia mema kutoka kwa mungu huyo.
Nyingi kati ya nywele bandia zinazouzwa barani Afrika huagizwa kutoka India,India ndilo taifa linalouza kiasi kikubwa zaidi cha nywele za binadamu duniani,nywele hizi zinazouzwa kutoka hekalu huitwa remi na inakisiwa kuwa bora zaidi duniani na wanasema kuwa nywele na bei ya juu zaidi ni ile iliyojikunja kiasili kutoka kwa kichwa cha mama na kila moja ya nywele huuzwa kwa dola 1200 hivi.



Kwahiyo sasa,baada ya nywele hizo kukatwa hekaluni husafirishwa hadi kiwanda cha kimataifa rahel mjini chenai,afisa mkuu wa kiwanda hiki anaelezea kuwa nywele hizi za binadamu hugeuzwa na kupambwa ili kuuzwa kama nywele za kofia(wigi),nywele hizi huwekwa pamoja kisha zinachukuliwa na kukaguliwa vyema na kwao huonekana kama dhahabu,kila sehemu ya nywele huonekana na thamani kubwa na hii ndio dhahabu yao.
Baada ya nywele hizi kupangwa huoshwa mara 12 na maji ili kuhakikisha zinasalia safi kama zilivyokuwa kwenye vichwa vya akina mama kisha zinaachwa kukauka na kufungwa tayari kwa kupelelekwa sokoni hasa za nchi za Afrika.
Hatua ya akina dada kutumia nywele wasizojua zitokako kama mapambo mfano hizi zitolewazo kama sadaka kwa mungu wa kihindu kisha kutengenezwa na kusafirishwa kwetu afrika zina athari kubwa sana katika maisha yao ya kiroho na kimwili pia na ndio maana tafiti nyingi zilizofanywa zinaonesha asilimia kubwa ya wanawake wengi hutekwa na mapepo,majini na roho zingine chafu ambapo kisababishi mojawapo ni kutumia/kuvaa baadhi ya mapambo ambayo hapo awali yalitolewa kwa miungu wapinga KRISTO.Kwahiyo mimi binafsi nawasihi akina dada mtafakar sana kuhusu mapambo hayo mtumiayo na mchukue maamuzi yatakayokuwa na tija katika maisha yenu na familia zenu. ASANTENI SANA!
NB;
Chanzo cha habari hii; BBC
Taarifa hii ni ya ukweli kabisa wala sio hadithi kama wengine wanavyodhani
Ingia link hii uone jinsi wanavyofanya:
Hair Sacrificed to Idols!? https://youtu.be/AuduHfSRFiA via YouTube