WATANZANIA wengi kama mimi tulikuwa tukisikia tu kuhusu Azimio au Tamko la Abuja na Sheria za Kiislamu. Azimio hilo lilifanyika nchini Nigeria katika mji wa Abuja, mwaka 1989 ndiyo maana linaitwa Azimio la Abuja. Jumatatu ya Machi 12, mwaka huu, katika pita pita mjini Nairobi nimebahatika kupata gazeti linaloitwa " The ministry".
Katika gazeti hilo nikaona kwa mbali neno "Abuja declaration and the Sharia law." Nikalinunua gazeti hilo. Baada ya kulisoma, nikaridhika na nikaunganisha na yanayotokea katika nchi yetu ya Tanzania, juu ya harakati za wenzetu Waislamu ikiwa ni utekelezaji wa tamko hilo muhimu la Abuja.
Tamko au Azimio la Abuja linahusu nini hasa? Kadiri ya maelezo katika internet na gazeti hilo, inaonekana wazi kuwa Azimio la Abuja ni tamko rasmi juu ya Uislamu barani Afrika (Islam in Africa). Kwa hivi tunaweza kusema au tunasema kwamba hili tamko lilitolewa katika kilele cha kongamano la Uislamu barani Afrika. Kongamano hili liliandaliwa na nchi 46 za Kiislamu zinazojulikana kama OIC (Organization of Islamic Conference).
Lengo la umoja huu ni kuuendeleza Uislamu barani Afrika, kutekeleza mikakati ya kiislamu na kutatua matatizo yanayolikabili Bara la Afrika kama vile ukimwi, kifua kikuu, njaa na majanga mengine. Lakini pia inasemekana hata kuona maadili yanafuatwa katika bara hili. Haya si mambo mabaya lakini swali la msingi ni; je, kwa kutumia sheria gani?
Inadaiwa kwamba katika yote hayo lengo kuu la OIC na hasa kupitia Azimio la Abuja ni kuona kwamba Bara lote la Afrika linakuwa la kiislamu. Huu ndiyo ukweli wa mambo na wala si uchochezi wala propaganda, ukitaka ukweli nenda tu kwenye internet utaupata najisomee maandishi mbalimbali juu ya umoja huo wa nchi za kiislamu, yaani OIC.
Kama mwandishi wa habari (mwanataaluma kamili) kazi yangu ni kuelimisha umma na si kuupotosha kamwe. Inaonekana wazi kwamba umoja huu wa nchi 46 za kiislamu, sijui kama Tanzania imejiunga au bado lakini OIC ndiyo mwakilishi na mzungumzaji wa masuala ya pamoja yanayohusu Waislamu barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.
Sehemu ya madhumuni ya OIC, kupitia Azimio au Tamko la Abuja ni; "kufuta katika hali zote imani ya dini isiyo ya kiislamu katika nchi wanachama. Na imani ambazo itabidi zifutwe ni dini ya kikristo, na nyinginezo ambazo hazikubaliani na imani ya kiislamu.
Kwa mantiki hii, ni dhahiri kwamba kama Tanzania itajiunga na Umoja huu wa nchi za kiislamu itabidi dini nyingine zisizokubalika kwa imani ya kiislamu basi zifutwe. Sasa swali; je, hapa kuna uhuru wa kuabudu kweli? Na kama nia ya kutaka Tanzania ijiunge huko ni dhahiri Katiba yetu ya Tanzania ni lazima ibadilishwe kwanza, kwa sababu kwa sasa hairuhusu.
Lakini kwa upande mwingine, madhara ya Azimio hili la Abuja tunayasikia mara nyingi nchini Nigeria ambako Wakristo wengi wamekwishauawa kikatili; je, hii ni halali?
Ukichunguza kwa kina unaweza kubaini kwamba utekelezaji wa Azimio la Abuja unakuja pole pole, hauna haraka. Na ninasema wazi kwamba katika uchunguzi wangu nchini Tanzania, mipango hii pia imeanza kutekelezwa kimya kimya na kwa uangalifu mkubwa sana.
Hata hivyo, kwa namna ya kipekee mambo yameshajulikana juu ya ajenda hii ya siri, Mungu hawezi kuruhusu jambo la namna hiyo kutokea katika ardhi ya Watanzania.
Alama za Azimio hilo la Abuja zimeshaanza kujitokeza kwa mbali katika nyanja mbalimbali nchini Tanzania na kwa hiyo, wale wanaoshabikia suala la Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) kwanza wajue malengo yake ni yapi. Na ni vema kujiuliza je, Katiba ya nchi yetu, historia ya nchi yetu, utamaduni wa nchi utaweza kuukaribisha umoja kama huo?
Misingi iliyowekwa na muasisi na Baba wa Taifa Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Julius K Nyerere ilikuwa ya busara, upendo, usawa, inayokuza haki na amani kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote. Sasa fikiria kama ni kweli lengo kuu ndilo hilo je, Azimio la Abuja lina maslahi gani kwa Watanzania wa leo hii? Kama nilivyosema sifanyi propaganda bali ni kutaka kuelimisha umma wa Watanzania kama mwandishi hii ndiyo kazi yangu, kuwapa watu mwanga wajue wanakwenda wapi.
Pia kama padre ni nabii wa kutahadharisha waumini na wananchi kwa ujumla juu ya mambo mbalimbali na kinyume cha hapo, wito wangu hautakuwa na maana kabisa.
Yesu aliwaambia mitume wake; "Ninyi ni chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu" (Mathayo 5: 13-16). Nisipotimiza wajibu huu kutoka kwa Bwana basi mimi nitakuwa sijitendei haki mbele ya mwenyezi Mungu na mbele ya Watanzania wenzangu ambao wengi hawajui nini kinaendelea kuhusiana na masuala ya jamii na siasa.
Namaliza kwa kusema kwamba, sisi Watanzania na Tanzania yetu ni vema tukaendelea kushikilia misingi iliyojengwa na Baba wa Taifa kama tunataka kuendelea kuishi kwa umoja, upendo, haki na amani.
Nitaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusiana na Azimio la Ubuja katika makala zijazo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki mawazo ya Mwalimu Nyerere, Mungu wabariki viongozi wa Tanzania. Nawatakieni uchaguzi Mwema huko Arumeru Mashariki, chagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni